Jumatano, 19 Novemba 2014

Kanuni za upokea muujiza.



Maombi,zaburi 1:8,uniombea nami nitakupa mataifakuwa urithi,na misho ya dunia kuwa milki yako.
                mathayo7:7,Ombeni nanyi mtapewa,tafuteni nanyi mtaona;bisheni nanyi mtafunguliwa.

Imani ,  waebrania11:1..basi imani ni  kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni pamoja ya  mambo  yasiyoonekana.
                warumi10:17 basi imani,chanzo chake ni kusikia;nakusikia huja kwa neno la kristo.

utii     mithali3:1 mwanangu usiisahau sheria yangu ,bali moyowako uzishike amri zangu.
kumbukumbu.Kumpenda BWANA MUNGU wako kuitii sauti yake ,na kushikamana naye kwani  hiyo ndiyo uzima wako na wingi wa siku zako,upate kukaa katika nchi aliowaapia baba zako,ibrahimu na isaka na yakobo kuwa atawapa.

Subira  Mungu wetu hachelewi wala hawahi..

Upendo   Mungu ni pendo anatupenda sisi sote yafaa kuwa na upendo ili tufanane naye yeye kama BABA na sisi tu WATOTO wake.UPENDO  ndiyo kipimo cha ukamilifu.

                                amani ya kristo iwe nanyi nyote.

Furaha ipatikanyo katika Yesu kristo


Mungu ndiye Jiwe la msaada wakati wa shida.

Mwangalie bwana Yesu wakati wa shida yako ukiweka imani kwake utaona anavyofanya njia mahali pasipo na njia...BARIKIWA MPENDWA.

Alhamisi, 6 Novemba 2014

jipange kwa mafanikio makubwa ili upate upate makubwa..

you think small you remain small....so you have to Think big in order to get big success

Baraka za MUNGU zinastawisha...


KUISHI KATIKA NENO LA MUNGU..

            sheria ya bwana ndiyo neno la MUNGU ukilishika na kutenda kwa jinsi anavyoagiza unafananishwa mti uliokando ya mto ambao hustawi na kuzaa matunda kwa wakati wake kwa sababu ndani ya neno kuna maji na jua linalostawisha maisha yako...

OMBA KWA AJIRI NCHI YETU YA TANZANIA !...

Ulinzi wa MUNGU wafaa sana katika nchi yetu ili atuepushe na vita vya ndani na nje,magonjwa,roho chafu za ukengeufu wa ushoga,na lesbiani,na mambo mengi ya hatari yaweze kuteketezwa na moto wa roho matakatifu na damu ya YESU...
omba ulalapo na uamkapo.....MUNGU AKUBARIKI...

KABIDHI KILA KITU KWA BWANA

Asante MUNGU akubariki kwa kusoma chapisho hili!!....

Jumatatu, 3 Novemba 2014

SPIRITUAL QUATES....

Heri maana yake baraka,kumbe basi baraka kwa yeyote anayemkumbuka mnyonge ,kwani naye atakumbukwa na  MUNGU wakati taabu yake.........NENO LA MUNGU LINAAGIZA... 

Alhamisi, 30 Oktoba 2014

UZIMA WA MILELE







UZIMA WA MILELE...
Uzima wa milele ni zawadi ambayo imetolewa bure(mshahara wa dhambi ni mauti karama(zawadi) ya MUNGU ni uzima wa milele) na MUNGU kwa wanadamu.na hii ni baada ya Mungu kuangalia duniani na kuona wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu na hatukufaa mbele zake.kwa sababu MUNGU ni wa UPENDO hakutaka atupoteze watoto wake na vilevile yeye ni mwenye haki (hawaachi wenye hatia bila adhabu) maana yake hakutaka kutuadhibu akaamua kumtuma mwanae Yesu kristo aje kutufundisha kweli ili tuwekwe huru kwasababu shetani aliudanganya ulimwengu tangu mwanzo.na YESU kristo ndiye MUNGU kudhihirika kwetu ili tupate uzima wa milele(tunaokolewa kuepushwa na jehanamu ya moto na kuupata uzima wa milele) na ambao ndiyo kweli aliyoileta yesu inayotuweka wanadamu huru kutoka katika mizigo ya dhambi nakutufanya tuishi si katika matakwa yetu wenyewe bali ni kuishi kwa kumsikiliza MUNGU aliyetuumba.Zawadi ya uzima wa milele tunaipokea kwa kutubu dhambi kupitia yesu kristo ili tupatanishwe na MUNGU aliyetuumba.   

JESUS SAVES...



 YOU HAVE TO AGREE WITH ME THAT JESUS SAVES…do you know why I say that?..
Its because he has given a power of the holy spirit that when you call his name you get healed, protected from the demons, and you open up the  door for the blessings from God….                               
Mwamini YESU uokolewe na upate Baraka ya uzima wa  milele..       
                                                                                                                              

                                                                                                         

                                                                                  
                                                           


                                                                                                                                                                limechapishwa na ndugu JOSHUA MKUNGILE

Jumapili, 26 Oktoba 2014

MAOMBI YANADHIHIRISHA KWAMBA TUNAMWAMINI MUNGU!.


I am talking about our prayers in JESUS`s name proves that we trust our awesame GOD(JEHOVA SHALOM)..

Jumatatu, 20 Oktoba 2014

HERI KUFANYA HAKI KULIKO MALI...

Yafaa nini uwe na kila kitu lakini mbele za Mungu huhesabiwi  haki? ni kazi bure kwa sababu mali haitufanyi tupate uzima wa milele bali ni kumkiri YESU kuwa bwana na mwokozi na kuishi katika kutii neno lake ndipo tutapata uzima wa milele.

ONESHA UPENDO KWA ADUI YAKO...

Neno linatufundisha kutomfanyia mabaya adui yako kwa kumcheka na kumuacha aanguke,kumbe yafaa kumjari na kumuombea mafanikio.
Ni njia ya kutii neno la MUNGU.

Ijumaa, 17 Oktoba 2014

SAFE SIDE



    
 UPANDE ULIOSALAMA KWAKO
Chagua upande uliosalama  katika maisha yako,
tunashauriana  kuwa katika upande ambao ni salama kwa sababu ni upande ambao huwa na ushindi.
Katika movie kuna stering na adui na mwisho wa siku stering hushinda na adui hushindwa,hata vitani kunakuwa na mwenye haki na asiye na haki kama vile Tanzania na Uganda Tanzania ilikuwa inadai haki yake iliyonyang`anywa na idi amini  mwisho wa siku tulishinda vita.
Hata katika  maisha ya kiroho kunapande mbili ambazo zinavita isiyoisha upande wa YESU na shetani.
Sasa ili uishi maisha yaliyosalama na utangaze ushindi maishani mwako  nakukaribisha upande wa YESU mwana wa MUNGU ambaye alishinda tangu kuzaliwa na akashinda kifo na yupo mpaka sasa  mfalme mwenye ufalme usioteteleka amepewa mamlaka na MUNGU mbinguni na dunia ndiye aliyezishika funguo za uzima wa milele.
 Achana na upande wa shetani ambaye alishashindwa tangu mwanzo na hana mbingu na anasubiri kuunguzwa katika jehanamu iwakayo moto.
Mpokee Yesu ili ushinde....


Alhamisi, 9 Oktoba 2014

DONT BE SCARED MY FRIEND....

kama Musa alivyomwamini MUNGU kwasababu alimwona alivyojidhihirisha kwake  kama kichaka kiwakacho moto na Mungu kumpa ahadi ya kuwa nae,alivyoshuhudia mapigo ambayo Mungu aliyadhihirisha kwa farao.

Pia alijua kwamba atawavusha katika bahari ya shamu ni kwa sababu alizishika shuhuda na aliamini.
usihofu juu ya lolote ushindi upo kwa yeyote aliyeliweka tumaini kwa MUNGU.bahari ya shamu kwako yawezekana ni kutopata ada ya masomo,ugonjwa,njaa,kutopata pesa au mateso ya aina yoyote amini aliyekuumba yupo na anayajua maisha yako. alikujua hata kabla mimba yako kutungwa  (yeremia ),vilevile anasema anatuwazia yaliyomema na makubwa.
weka imani yako kwa YESU na ulishike neno lake kwasababu ndiko ziliko ahadi zake  na shuhuda zake utapokeaushindi.
ukiweka hofu juu ya matatizo utashindwa mfano petro aliamini atatembea juu ya maji akaweza alipoanza kuangalia mawimbi na ukubwa wa bahari hofu ilianza kuingia na imani kupungua akaanza kuzama katika maji.
na wewe usiangalie ukubwa wa tatizo muangalie Mungu aliyemkuu(mkubwa) na muweza wa yote utashinda ..
AMINI NA ULISHIKE NENO LAKE UTASHINDA USIANGALIE UKUBWA WA TATIZO.
MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUPITIA CHAPISHO HILI...

Jumamosi, 27 Septemba 2014

mwokozi wetu YESU..






                                         Mwamini Yesu upatanishwe na MUNGU aliyekuumba..

Jumamosi, 13 Septemba 2014

SILAHA ZA VITA KATIKA MAISHA YA KIROHO.



             SILAHA ZA VITA KATIKA MAISHA YA KIROHO.

Silaha ni vifaa vinavyotumika wakati wa vita na kuleta ushindi.

Mpendwa unapompokea Yesu kuwa bwana mwokozi wa maisha yako na kuanza kuishi maisha ya kiroho unakuwa umetangaza vita katika ulimwengu wa roho.maana yake umeokolewa kutoka katika mikono ya shetani kuanzia hapo shetani anaanza kukutafuta ili akurudishe kwenye ulimwengu wa kipepo ili uukose uzima wa milele.na kama ndiyo umeokoka tu vita huanza kupitia watu wako wajirani na wa muhim ili kukuyumbisha mfano vita huanza kupitia wazazi kutokubaliana na maamuzi yako na kukufukuza au kutokukusomesha na vitisho vya aina nyingi ili ukate tamaa.usikate tamaa kwa sababu ya majaribu kwa sababu Mungu hukutana na watoto wake wakati wa matatizo.hata Yesu mwenyewe alikatariwa tangu yupo tumboni hata mariam akakosa mahali pa kujihifadhi ni vita za shetani kuharibu kusudi la Mungu lakini kwa sababu Mungu ni mwenye kutunza ahadi na ni wa ushindi Yesu alizaliwa na na aliitangaza kweli na alinyeyekea mpaka mwisho na sasa kainuliwa yupo upande wa kuume wa MUNGU BABA na amepewa mamlaka.USIKATE TAMAA  YASHINDE MAJARIBU ILI UINULIWE.

Leo nataka tujifunze baadhi ya silaha za vita tulizopewa na Mungu ili tushinde.


Efeso 6:14,basi simameni,hali mmejifunga kweli viunoni na kuvaa dirii ya ya haki kifuani,na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa injiri ya amani,zaidi ya yote mkiitwa ngao ya imani ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya Yule mwovu. Sehem zilizopigiwa mstari ni silaha ambazo zinakuwezesha kutangaza ushuhuda wa kweli na ushindi.

·         Kweli humfanya mtu kuwa huru na ukisha kuwa huru  vita lazima utavishinda maana yake hauna jambo lolota linalokufanya usijiamini,haki ni uhusiano mzui yrtu na mungu,nyoofu wa kweli mbele za Mungu

·         Neno la Mungu,efeso6:17 neno la Mungu ni upanga wa roho linakata kila aina ya uharibifu unaotaka kumpoteza mtu katika maisha ya kiroho.yeremia23:29 je! neno langu si kama moto?aseme bwana na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande. Mathayo4:3 Pia shetani alimjaribu Yesu lakini kwa sababu Yesu alijawa na neno la Mungu alimshinda shetani kwamba mtu haishi kwa mkate tu ila ni kwa neno litokalokatika kinywa cha Mungu.kumbe neno   la Mungu ni uzima na ni njia ya kumshinda mwovu.usipokuwa na neno la Mungu, utamjibu mwenzio vibaya,utatukana,utakata tamaa kwa sababu ya vitisho vya mwovu.soma neno la Mungu umshinde shetani.

·        
Jina la Yesu,tunatakiwa kulitumia jina la yesu katika vita ili kuharibu majeshi maelfu ya shetani,pia kufungua Baraka,kupatanishwa na Mungu,katika kila jambo tunalolifanya yafaa liwe katika jina la yeu ndipo tutamwona Mungu akitushindia.(tunalitumia jina la Yesu ili Baba yaani (MUNGU) atukuzwe kupitia mwana ambaye ndiye Yesu).(filipi2:9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno,akamkirimia jina lile lipitalo kila jina ,ili kwa jina la yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni na vya duniani,na vya chini ya nchi.na kila ulimi ukiri ya kuwa ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA,kwa utukufu wa MUNGU BABA)Mungu alimpa jina ambalo litafanyika ushindi kwa wote watakao mwamini.

·         Damu ya Yesu,ufunuo wa yohana12:11 Nao wakamshinda kwa damu ya mwana kondoo na kwa neno la ushuhuda wao…kumbe tunashinda vita kwa damu ya mwana kondoo nae Yesu kristo,

·         Sifa kuu ni silaha,kumsifu Mungu kwa roho na kweli ni silaha kwa sababu kunakaribisha nguvu ya  roho mtakatifu.kupitia roho mtakatifu matando16:25-26 Paulo na sila waliomba na kumsifu Mungu mpaka milango ya gereza ikafunguka.ni kwa sababu ya sifa iliyo ya kweli na kupitia sifa watu hupata nguvu ya kufanya maombi bila kuchoka.kama mpendwa yakupasa uombee ibada ya sifa kila unapoingia ibadani ili umuone Mungu akifungua watu na kuponya watu na kunena na kanisa.

·         Radi ya Mungu,ina maanisha tupo katika ufalme usioteteleka zaburi18:13bwana alipiga radi mbinguni,yeye aliye juu akaitoa sauti yake) ,1samweli2:10(washindanao na BWANA watapondwa kabisa toka mbinguni yeye atawapigia radi) kumbe Mungu tunayemwamini ni mtetezi wetu wakati wa vita adui atakapojipanga kutupiga atasambalatishwa kwa Radi kutoka kwa MUNGU.

Matumizi ya silaha hizi yapo katika maombi na kuhudhuria ibada kwa bidii.

hivyo ninashauri utumie bidii ya hali ya juu sana katika maombi ya kawaida na kufunga mara nyingi angalau mara mbili kwa wiki au mara tatu au zaidi maana adui shetani halali vivyo nasi tusifanye kwa ulegevu.

Pia yatupasa tuhudhurie ibada isiwepo sababu yoyote yakutufanya tusiende ibadani.

Hizi ni moja silaha zinazokupa ushindi na kukufanya usimame imara  ukimtegemea MUNGU katika maisha ya kiroho.

                            MUNGU akubariki kwa kusoma ujumbe huu…




+