Chagua
upande uliosalama katika maisha yako,
tunashauriana kuwa katika upande ambao ni salama kwa sababu
ni upande ambao huwa na ushindi.
Katika
movie kuna stering na adui na mwisho wa siku stering hushinda na adui
hushindwa,hata vitani kunakuwa na mwenye haki na asiye na haki kama vile
Tanzania na Uganda Tanzania ilikuwa inadai haki yake iliyonyang`anywa na idi
amini mwisho wa siku tulishinda vita.
Hata
katika maisha ya kiroho kunapande mbili
ambazo zinavita isiyoisha upande wa YESU na shetani.
Sasa ili
uishi maisha yaliyosalama na utangaze ushindi maishani mwako nakukaribisha upande wa YESU mwana wa MUNGU ambaye alishinda tangu kuzaliwa na akashinda kifo na yupo
mpaka sasa mfalme mwenye ufalme
usioteteleka amepewa mamlaka na MUNGU mbinguni na dunia ndiye aliyezishika
funguo za uzima wa milele.
Achana na upande wa shetani ambaye alishashindwa tangu mwanzo na hana
mbingu na anasubiri kuunguzwa katika jehanamu iwakayo moto.
Mpokee Yesu ili ushinde....
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni