SILAHA ZA VITA KATIKA MAISHA YA KIROHO.
Silaha ni vifaa vinavyotumika wakati wa vita na
kuleta ushindi.
Mpendwa unapompokea Yesu kuwa bwana mwokozi wa
maisha yako na kuanza kuishi maisha ya kiroho unakuwa umetangaza vita katika
ulimwengu wa roho.maana yake umeokolewa kutoka katika mikono ya shetani kuanzia
hapo shetani anaanza kukutafuta ili akurudishe kwenye ulimwengu wa kipepo ili
uukose uzima wa milele.na kama ndiyo umeokoka tu vita huanza kupitia watu wako
wajirani na wa muhim ili kukuyumbisha mfano vita huanza kupitia wazazi
kutokubaliana na maamuzi yako na kukufukuza au kutokukusomesha na vitisho vya
aina nyingi ili ukate tamaa.usikate tamaa kwa sababu ya majaribu kwa sababu
Mungu hukutana na watoto wake wakati wa matatizo.hata Yesu mwenyewe alikatariwa
tangu yupo tumboni hata mariam akakosa mahali pa kujihifadhi ni vita za shetani
kuharibu kusudi la Mungu lakini kwa sababu Mungu ni mwenye kutunza ahadi na ni
wa ushindi Yesu alizaliwa na na aliitangaza kweli na alinyeyekea mpaka mwisho na
sasa kainuliwa yupo upande wa kuume wa MUNGU BABA na amepewa mamlaka.USIKATE
TAMAA YASHINDE MAJARIBU ILI UINULIWE.
Leo
nataka tujifunze baadhi ya silaha za vita tulizopewa na Mungu ili tushinde.
Efeso
6:14,basi
simameni,hali mmejifunga kweli viunoni na kuvaa dirii ya ya haki kifuani,na
kufungiwa miguu utayari tupatao kwa injiri ya amani,zaidi ya yote
mkiitwa ngao ya imani ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye
moto ya Yule mwovu. Sehem zilizopigiwa
mstari ni silaha ambazo zinakuwezesha kutangaza ushuhuda wa kweli na ushindi.
·
Kweli humfanya mtu kuwa huru na ukisha
kuwa huru vita lazima utavishinda maana
yake hauna jambo lolota linalokufanya usijiamini,haki ni uhusiano mzui yrtu na
mungu,nyoofu wa kweli mbele za Mungu
·
Neno la Mungu,efeso6:17 neno la Mungu ni upanga wa roho linakata kila aina ya
uharibifu unaotaka kumpoteza mtu katika maisha ya kiroho.yeremia23:29
je! neno langu si kama moto?aseme bwana na kama nyundo ivunjayo mawe vipande
vipande. Mathayo4:3 Pia shetani alimjaribu Yesu lakini kwa sababu Yesu
alijawa na neno la Mungu
alimshinda shetani kwamba mtu haishi kwa mkate tu ila ni kwa neno
litokalokatika kinywa cha Mungu.kumbe neno la Mungu ni uzima na ni njia ya kumshinda
mwovu.usipokuwa na neno la Mungu, utamjibu mwenzio vibaya,utatukana,utakata
tamaa kwa sababu ya vitisho vya mwovu.soma neno la Mungu umshinde shetani.
·
Jina la Yesu,tunatakiwa kulitumia jina
la yesu katika vita ili kuharibu majeshi maelfu ya shetani,pia kufungua
Baraka,kupatanishwa na Mungu,katika kila jambo tunalolifanya yafaa liwe katika
jina la yeu ndipo tutamwona Mungu akitushindia.(tunalitumia
jina la Yesu ili Baba yaani (MUNGU) atukuzwe kupitia mwana ambaye ndiye Yesu).(filipi2:9 Kwa hiyo tena
Mungu alimwadhimisha mno,akamkirimia jina lile lipitalo kila jina ,ili kwa jina
la yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni na vya duniani,na vya chini ya
nchi.na kila ulimi ukiri ya kuwa ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA,kwa utukufu wa
MUNGU BABA)Mungu alimpa jina ambalo litafanyika ushindi kwa wote
watakao mwamini.
·
Damu ya Yesu,ufunuo wa yohana12:11 Nao
wakamshinda kwa damu ya mwana kondoo na kwa neno la ushuhuda wao…kumbe
tunashinda vita kwa damu ya mwana kondoo nae Yesu kristo,
·
Sifa kuu ni silaha,kumsifu Mungu kwa
roho na kweli ni silaha kwa sababu kunakaribisha nguvu ya roho mtakatifu.kupitia roho mtakatifu matando16:25-26 Paulo na sila waliomba na kumsifu Mungu
mpaka milango ya gereza ikafunguka.ni kwa sababu ya sifa iliyo ya kweli na
kupitia sifa watu hupata nguvu ya kufanya maombi bila kuchoka.kama mpendwa yakupasa
uombee ibada ya sifa kila unapoingia ibadani ili umuone Mungu akifungua watu na
kuponya watu na kunena na kanisa.
·
Radi ya Mungu,ina maanisha tupo katika
ufalme usioteteleka zaburi18:13bwana alipiga radi mbinguni,yeye aliye juu akaitoa sauti
yake) ,1samweli2:10(washindanao na BWANA watapondwa kabisa toka mbinguni yeye
atawapigia radi) kumbe Mungu tunayemwamini ni mtetezi wetu wakati wa
vita adui atakapojipanga kutupiga atasambalatishwa kwa Radi kutoka kwa MUNGU.
Matumizi ya silaha hizi
yapo katika maombi na kuhudhuria ibada kwa bidii.
hivyo ninashauri utumie
bidii ya hali ya juu sana katika maombi ya kawaida na kufunga mara nyingi
angalau mara mbili kwa wiki au mara tatu au zaidi maana adui shetani halali
vivyo nasi tusifanye kwa ulegevu.
Pia yatupasa tuhudhurie
ibada isiwepo sababu yoyote yakutufanya tusiende ibadani.
Hizi ni moja silaha zinazokupa ushindi na kukufanya usimame
imara ukimtegemea MUNGU katika maisha ya
kiroho.
MUNGU akubariki kwa
kusoma ujumbe huu…
+
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni