Alhamisi, 4 Septemba 2014

NJIA YA KWELI KUPATANISHWA NA MUNGU





Nakusalimu mpendwa katika jina la Yesu…..Ni siku nyingine ambayo tunaendelea kushirikishana neno la MUNGU.

Leo tutakumbushana kitu kimoja ambacho watu wengi hatujakijua vizuri au yawezekana

tunakijua lakini twapuuza ukweli unaowekwa wazi.Kila mtu ana IMANI Fulani juu ya Mungu anayemwamini wengine Mungu jua,ng`ombe,bhudha na mengineyo na kuna wapagani vilevile.

Lakini kitu kimoja kiwe wazi kwamba MUNGU wa kweli ni mmoja tu naye ndiye alieumba mbingu na nchi na vitu vyote vilivyomo na kujidhihirisha kwetu wanadamu kupitia YESU KRISTO

(Yohana 14:6 Yesu akamwambia mimi ndimi njia, na kweli, na uzimamtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi.)neno lipo wazi kwamba humfikii MUNGU bila kutubu kupitia Yesu.na hata katika ulimwengu wa roho kuna pande mbili tu ni MUNGU Vs shetani

 Usipomwamini  Yesu kristo kuwa bwana na mwokozi wako hutaingia mbinguni na ni dalili tosha haupo ktk imani ya kweli.

Mungu wa kweli ni mmoja tu hii miungu mingine ni ujanja  ambao shetani anautumia kuudanganya ulimwengu na kuwafanya watu  wasiipate imani ya kweli.

Matendo16:31…biblia inasema`wakamwambia, mwamini yesu utaokoka pamoja na nyumba yako.imani ni hali ya kutegemea kama ombaomba anavyotegemea kupewa na watu kwa kunyoosha mikono miwili.neno latufundisha kuamini(kutegemea)katika bwana Yesu ndipo tutaokolewa.badili imani(utegemezi) wako leo mwamini YESU KRISTO upatanishwe na MUNGU na ndiyo njia pekee ya kupokea zawadi ya UZIMA WA MILELE.(Ufunuo wa yohana3:20 Tazama nasimama mlangoni ,nabisha,mtu akiisikia sauti yangu ,nakuufungua mlango,nitaingia kwake.JE UNGEPENDA KUMKARIBISHA YESU AINGIE MAISHANI MWAKO NAKUWA MWOKOZI WAKO?....

SEMA MANENO HAYA…Baba wa mbinguni,nimeishi maisha yangukwa njia yangu.nimefanya mambo mengi mabaya,ninatubu dhambi zangu zote.naomba unisamehe,sasa ninakuamini wewe mwokozi wangu,asante kwa kufa kwa ajiri yangu,ninakuomba sasa unipe zawadi ya uzima wa milele.ninatoa maisha yangu kwako, nami ninataka uwe mwokozi wangu, nisaidie kuishi kwa ajiri yako kwa nguvu ya roho mtakatifu katika jina la YESU.. amina.

Tafuta sehemu yoyote yenye makanisa ya kipentekoste upate mafundisho… MUNGU AKUBARIKI SANA…


Maoni 1 :