Alhamisi, 30 Oktoba 2014

UZIMA WA MILELE







UZIMA WA MILELE...
Uzima wa milele ni zawadi ambayo imetolewa bure(mshahara wa dhambi ni mauti karama(zawadi) ya MUNGU ni uzima wa milele) na MUNGU kwa wanadamu.na hii ni baada ya Mungu kuangalia duniani na kuona wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu na hatukufaa mbele zake.kwa sababu MUNGU ni wa UPENDO hakutaka atupoteze watoto wake na vilevile yeye ni mwenye haki (hawaachi wenye hatia bila adhabu) maana yake hakutaka kutuadhibu akaamua kumtuma mwanae Yesu kristo aje kutufundisha kweli ili tuwekwe huru kwasababu shetani aliudanganya ulimwengu tangu mwanzo.na YESU kristo ndiye MUNGU kudhihirika kwetu ili tupate uzima wa milele(tunaokolewa kuepushwa na jehanamu ya moto na kuupata uzima wa milele) na ambao ndiyo kweli aliyoileta yesu inayotuweka wanadamu huru kutoka katika mizigo ya dhambi nakutufanya tuishi si katika matakwa yetu wenyewe bali ni kuishi kwa kumsikiliza MUNGU aliyetuumba.Zawadi ya uzima wa milele tunaipokea kwa kutubu dhambi kupitia yesu kristo ili tupatanishwe na MUNGU aliyetuumba.   

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni