Jumamosi, 13 Septemba 2014

USIHARIBU MAISHA YAKO YA KIROHO



Shalom wapendwa….


Poleni na shughuri za mahangaiko ya kimaisha.
Leo nitaongelea kutoharibu maisha ya kiroho  baada yakumpokea  Yesu kuwa bwana na mwokozi wa maisha yetu.
 kutoharibu mfumo wa maisha ya kiroho tulioyapata kwa gharama ya kumwagika kwa damu ya Yesu isiyo na hatia kwa ajiri yetu.
Inabidi tuujari wokovu tuliopewa na Mungu,waebrania2:3 sisi je? tutapate kupona tusipoujari wokovu mkuu namna hii?
Wote twajua kwamba aliteswa kama mwizi anapopigwa kwa nyakati za sasa  mpaka kuchomwa moto na kwa zamani mwizi au mharifu alipigwa na kuwekwa msalabani.
Ukifikiria kwamba aliyepigwa ni MWANA WA MUNGU kwa ajiri yetu tusipate adhabu ya jehanamu kitu gani kikutenganishe wewe leo na ufalme wa MUNGU.
Usiruhusu kitu chochote kikuharibie ushirika na Mungu,shetani anafanya kazi katika njia nyingi kututengenisha na upendo wa Mungu.(1Petro5:8,mwe na kiasi na kukesha ;kwa kuwa mshitaki wenu ibirisi kama samba angurumaye,huzunguka zunguka akitafuta mtu ammeze.nanyi mpingeni huyo mkiwa dhabiti katika imani  mkijua ya kuwa mateso yaleyale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani ) . anapitia uchumi wetu,masomo,ndoa,marafiki,hata mitandao lakini fikiria Mungu yupo mwenye uwezo zaidi kutufanya tushinde.nyenyekea hata wakati wa majaribu ili umuone Mungu.(1Petro basi nyeyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari,ili awakweze kwa wakati wake).
Mtumainie bwana Yesu siku zote ili usiaibike maishani mwako…
AMANI IWE NANYI NA MUNGU AWABARIKI..


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni