Alhamisi, 9 Oktoba 2014

DONT BE SCARED MY FRIEND....

kama Musa alivyomwamini MUNGU kwasababu alimwona alivyojidhihirisha kwake  kama kichaka kiwakacho moto na Mungu kumpa ahadi ya kuwa nae,alivyoshuhudia mapigo ambayo Mungu aliyadhihirisha kwa farao.

Pia alijua kwamba atawavusha katika bahari ya shamu ni kwa sababu alizishika shuhuda na aliamini.
usihofu juu ya lolote ushindi upo kwa yeyote aliyeliweka tumaini kwa MUNGU.bahari ya shamu kwako yawezekana ni kutopata ada ya masomo,ugonjwa,njaa,kutopata pesa au mateso ya aina yoyote amini aliyekuumba yupo na anayajua maisha yako. alikujua hata kabla mimba yako kutungwa  (yeremia ),vilevile anasema anatuwazia yaliyomema na makubwa.
weka imani yako kwa YESU na ulishike neno lake kwasababu ndiko ziliko ahadi zake  na shuhuda zake utapokeaushindi.
ukiweka hofu juu ya matatizo utashindwa mfano petro aliamini atatembea juu ya maji akaweza alipoanza kuangalia mawimbi na ukubwa wa bahari hofu ilianza kuingia na imani kupungua akaanza kuzama katika maji.
na wewe usiangalie ukubwa wa tatizo muangalie Mungu aliyemkuu(mkubwa) na muweza wa yote utashinda ..
AMINI NA ULISHIKE NENO LAKE UTASHINDA USIANGALIE UKUBWA WA TATIZO.
MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUPITIA CHAPISHO HILI...

Maoni 1 :