Alhamisi, 30 Oktoba 2014

UZIMA WA MILELE







UZIMA WA MILELE...
Uzima wa milele ni zawadi ambayo imetolewa bure(mshahara wa dhambi ni mauti karama(zawadi) ya MUNGU ni uzima wa milele) na MUNGU kwa wanadamu.na hii ni baada ya Mungu kuangalia duniani na kuona wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu na hatukufaa mbele zake.kwa sababu MUNGU ni wa UPENDO hakutaka atupoteze watoto wake na vilevile yeye ni mwenye haki (hawaachi wenye hatia bila adhabu) maana yake hakutaka kutuadhibu akaamua kumtuma mwanae Yesu kristo aje kutufundisha kweli ili tuwekwe huru kwasababu shetani aliudanganya ulimwengu tangu mwanzo.na YESU kristo ndiye MUNGU kudhihirika kwetu ili tupate uzima wa milele(tunaokolewa kuepushwa na jehanamu ya moto na kuupata uzima wa milele) na ambao ndiyo kweli aliyoileta yesu inayotuweka wanadamu huru kutoka katika mizigo ya dhambi nakutufanya tuishi si katika matakwa yetu wenyewe bali ni kuishi kwa kumsikiliza MUNGU aliyetuumba.Zawadi ya uzima wa milele tunaipokea kwa kutubu dhambi kupitia yesu kristo ili tupatanishwe na MUNGU aliyetuumba.   

JESUS SAVES...



 YOU HAVE TO AGREE WITH ME THAT JESUS SAVES…do you know why I say that?..
Its because he has given a power of the holy spirit that when you call his name you get healed, protected from the demons, and you open up the  door for the blessings from God….                               
Mwamini YESU uokolewe na upate Baraka ya uzima wa  milele..       
                                                                                                                              

                                                                                                         

                                                                                  
                                                           


                                                                                                                                                                limechapishwa na ndugu JOSHUA MKUNGILE

Jumapili, 26 Oktoba 2014

MAOMBI YANADHIHIRISHA KWAMBA TUNAMWAMINI MUNGU!.


I am talking about our prayers in JESUS`s name proves that we trust our awesame GOD(JEHOVA SHALOM)..

Jumatatu, 20 Oktoba 2014

HERI KUFANYA HAKI KULIKO MALI...

Yafaa nini uwe na kila kitu lakini mbele za Mungu huhesabiwi  haki? ni kazi bure kwa sababu mali haitufanyi tupate uzima wa milele bali ni kumkiri YESU kuwa bwana na mwokozi na kuishi katika kutii neno lake ndipo tutapata uzima wa milele.

ONESHA UPENDO KWA ADUI YAKO...

Neno linatufundisha kutomfanyia mabaya adui yako kwa kumcheka na kumuacha aanguke,kumbe yafaa kumjari na kumuombea mafanikio.
Ni njia ya kutii neno la MUNGU.

Ijumaa, 17 Oktoba 2014

SAFE SIDE



    
 UPANDE ULIOSALAMA KWAKO
Chagua upande uliosalama  katika maisha yako,
tunashauriana  kuwa katika upande ambao ni salama kwa sababu ni upande ambao huwa na ushindi.
Katika movie kuna stering na adui na mwisho wa siku stering hushinda na adui hushindwa,hata vitani kunakuwa na mwenye haki na asiye na haki kama vile Tanzania na Uganda Tanzania ilikuwa inadai haki yake iliyonyang`anywa na idi amini  mwisho wa siku tulishinda vita.
Hata katika  maisha ya kiroho kunapande mbili ambazo zinavita isiyoisha upande wa YESU na shetani.
Sasa ili uishi maisha yaliyosalama na utangaze ushindi maishani mwako  nakukaribisha upande wa YESU mwana wa MUNGU ambaye alishinda tangu kuzaliwa na akashinda kifo na yupo mpaka sasa  mfalme mwenye ufalme usioteteleka amepewa mamlaka na MUNGU mbinguni na dunia ndiye aliyezishika funguo za uzima wa milele.
 Achana na upande wa shetani ambaye alishashindwa tangu mwanzo na hana mbingu na anasubiri kuunguzwa katika jehanamu iwakayo moto.
Mpokee Yesu ili ushinde....


Alhamisi, 9 Oktoba 2014

DONT BE SCARED MY FRIEND....

kama Musa alivyomwamini MUNGU kwasababu alimwona alivyojidhihirisha kwake  kama kichaka kiwakacho moto na Mungu kumpa ahadi ya kuwa nae,alivyoshuhudia mapigo ambayo Mungu aliyadhihirisha kwa farao.

Pia alijua kwamba atawavusha katika bahari ya shamu ni kwa sababu alizishika shuhuda na aliamini.
usihofu juu ya lolote ushindi upo kwa yeyote aliyeliweka tumaini kwa MUNGU.bahari ya shamu kwako yawezekana ni kutopata ada ya masomo,ugonjwa,njaa,kutopata pesa au mateso ya aina yoyote amini aliyekuumba yupo na anayajua maisha yako. alikujua hata kabla mimba yako kutungwa  (yeremia ),vilevile anasema anatuwazia yaliyomema na makubwa.
weka imani yako kwa YESU na ulishike neno lake kwasababu ndiko ziliko ahadi zake  na shuhuda zake utapokeaushindi.
ukiweka hofu juu ya matatizo utashindwa mfano petro aliamini atatembea juu ya maji akaweza alipoanza kuangalia mawimbi na ukubwa wa bahari hofu ilianza kuingia na imani kupungua akaanza kuzama katika maji.
na wewe usiangalie ukubwa wa tatizo muangalie Mungu aliyemkuu(mkubwa) na muweza wa yote utashinda ..
AMINI NA ULISHIKE NENO LAKE UTASHINDA USIANGALIE UKUBWA WA TATIZO.
MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUPITIA CHAPISHO HILI...