Nakusalimu
mpendwa katika jina la Yesu…..Ni siku nyingine ambayo tunaendelea
kushirikishana neno la MUNGU.
Leo
tutakumbushana kitu kimoja ambacho watu wengi hatujakijua vizuri au yawezekana
tunakijua lakini twapuuza ukweli unaowekwa wazi.Kila
mtu ana IMANI Fulani juu ya Mungu anayemwamini wengine Mungu jua,ng`ombe,bhudha
na mengineyo na kuna wapagani vilevile.
Lakini kitu kimoja kiwe wazi kwamba MUNGU wa kweli
ni mmoja tu naye ndiye alieumba mbingu na nchi na vitu vyote vilivyomo na
kujidhihirisha kwetu wanadamu kupitia YESU KRISTO
(Yohana 14:6 Yesu akamwambia mimi ndimi njia, na kweli, na
uzimamtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi.)neno lipo wazi kwamba humfikii
MUNGU bila kutubu kupitia Yesu.na hata katika ulimwengu wa roho kuna
pande mbili tu ni MUNGU Vs shetani
Usipomwamini Yesu kristo kuwa bwana na mwokozi wako
hutaingia mbinguni na ni dalili tosha haupo ktk imani ya kweli.
Mungu wa kweli ni mmoja tu hii miungu mingine ni
ujanja ambao shetani anautumia
kuudanganya ulimwengu na kuwafanya watu wasiipate
imani ya kweli.
Matendo16:31…biblia inasema`wakamwambia,
mwamini yesu utaokoka pamoja na nyumba yako.imani ni hali
ya kutegemea kama ombaomba anavyotegemea kupewa na watu kwa kunyoosha mikono
miwili.neno latufundisha kuamini(kutegemea)katika bwana Yesu ndipo
tutaokolewa.badili imani(utegemezi) wako leo mwamini YESU KRISTO upatanishwe na
MUNGU na ndiyo njia pekee ya kupokea zawadi ya UZIMA WA MILELE.(Ufunuo wa yohana3:20 Tazama nasimama mlangoni ,nabisha,mtu akiisikia
sauti yangu ,nakuufungua mlango,nitaingia kwake.JE UNGEPENDA KUMKARIBISHA YESU AINGIE MAISHANI MWAKO NAKUWA
MWOKOZI WAKO?....
SEMA MANENO HAYA…Baba wa mbinguni,nimeishi maisha yangukwa njia yangu.nimefanya
mambo mengi mabaya,ninatubu dhambi zangu zote.naomba unisamehe,sasa ninakuamini
wewe mwokozi wangu,asante kwa kufa kwa ajiri yangu,ninakuomba sasa unipe zawadi
ya uzima wa milele.ninatoa maisha yangu kwako, nami ninataka uwe mwokozi wangu,
nisaidie kuishi kwa ajiri yako kwa nguvu ya roho mtakatifu katika jina la
YESU.. amina.
Tafuta sehemu yoyote yenye makanisa ya
kipentekoste upate mafundisho… MUNGU AKUBARIKI SANA…
mnakaribishwa kwa maoni au maswali....
JibuFuta